I Love

Khadija Kopa

Hawana wema wanadamu
Wana fitina wanadamu
Wanadamu, wanadamu
Wana hamu ya kutudhulumu

Hauishi hamu penzi litadumu
Kwa nguvu za Karima, daima dawamu
Hauishi hamu penzi litadumu
Kwa nguvu za Karima, daima dawamu

Hawana wema wanadamu
Hawana jema wanadamu
Hawana wema wanadamu
Hawana jema wanadamu

Habibi wangu muhimu
Sogea nikupe raha
Kukusalimu nina hamu
Vipi ulivyoamka?

Ni mzima mahashumu
Mmefurahi bila shaka
Haishi yangu hamu
Mapenzi sijatosheka

Kato sitokudhulumu
Mwenzio nakutaka
Tulia wangu muhangamu
Kwenye huba umefika

Raha zangu mie tamu
Mapenzi ya pata shika
Na wala sitokulaumu
Nitakupa sitochoka

I love you, baby
I love you, baby
I love you, baby
I love you, baby

Tutulie ili tuwaonyeshe
Washuhudie wapate kasheshe
Tutulie ili tuwaonyeshe
Washuhudie wapate kasheshe

Nakupenda kweli kweli
Nakuzimikia kweli
Nakupenda kweli kweli
Nakuzimikia kweli

I love you, I love you
I love you, I love you
I miss you, I miss you
I miss you forever and ever

Mpenzi kuwa timamu
Uko nje ukitoka
Watu hali ya hakimu
Na wao watalitaka

Wivu kwako ndio sumu
Siwahi kukuepuka
Kwangu wewe ndio mtamu
Robo hawakufika

Mimi sitokudhulumu
Wakitaka, sitotaka
Hutonitia wazimu
Nishazowea kudeka

Utanitia wazimu
Uko nje ukitoka
Pendo lataka nidhamu
Usiwape waja kucheka

Utanitia wazimu
Nishazoe akudeka
Pendo lataka nidhamu
Usiwape waja kucheka

Kukupenda nilazima
Wewe wangu natamka
Wasikutie wazimu
Hakuna nilomtaka

Na mimi sikulaumu
Kupendwa ndo nataka
Na yanhu yalazimu
Sisemi siri naweka


All lyrics are property and copyright of their owners. All lyrics provided for educational purposes only.